PICHA: EVENT YA AFYA KWANZA - JOSAM HOUSE, TAREHE 17.1. 2015

 Mnamo tarehe 17.1.2015 Siku ya Jumamosi Maza Senare Mchome "Maznat" aliandaa bonge la event kwa ajili ya kuwakumbusha na kuwahimiza wadau kuhusu umuhimu wa afya hususani katika kufanya mazoezi kila mara na kuzingatia kula vema "healthy eating". Yeye Maza alizungumzia kwa kina jinsi ya kufanya diet yenye mpangilio na inayomsaidia mtu kupunguza unene na kuwa fit, Dr. Mwaka alizungumzia athari za unene kwenye mfumo wa uzazi wa wanawake na mimi (Dr. Chris Mauki) nikamalizia kuzungumzia athari za unene, uzito wa ziada na kitambi kwenye yale mambo yetu yaleeeeeeeeeeeeee ".....tendo la ndoa". Kiukweli palikuwa njema sanaaaaa. Pichani ni My Miriam na Maza mara baada ya Event kumalizika
 Hapa nikidadavua point, na wadau wakiwa makini sana kunifuatilia
 Upako wa kufundisha ukanishukia, it was really good
 Baada ya event wadau mbali mbali walikuwa na kiu ya kupata japo picha za ukumbusho
 Teaching ikiendelea kama kawa, kwambali namwona Maza kadata kwa kicheko, hajiwezi kabisa

 Rafiki yangu, my brother Dr. Mwaka wengi mnamsikia na kumwona kwenye luninga na redioni, alikuwa akifafanua jinsi ambavyo unene unaathiri mfumo wa uzazi na afya nzima ya mwanadamu hususani mwanamke
 Kama kawa, shule ikimwagika na wadau wakifaidika nayo
 Dr. Mwaka na Maza nao hawakupitwa na nondo zilizokuwa zinateremka
 Mi ninamjua na kumfahamu huyu, sijui wewe??
 Maza kutoka Maznat Bridal Care Mikocheni akifundisha kwa umakini mkubwa, shule yake ilikuwa msaada sana kwa wengi


 Yuleeeeeeeeeee
 Nimekuwa nikimtumia kwenye mifano mara kwa mara nikifundisha, hapa nikikuwa natoa mfano wa namna Miriam (Mke wangu) alivyowahi kuwa na umbo na uzito mkubwa na jinsi alivyoweka jitihada kuhakikisha anapungua, na pia faida ambazo anaziona kwa sasa.

 Dr. Chris Mauki, Maza, Miriam, na Sara Mauki (Mdogo wangu wa tatu) hapa ni baada ya event kuisha kila mtu akiwa amejaa furaha kwa mafunzo
 Dr. Mwaka na Dr. Chris Mauki

 An angel in the midst of others

 Miriam na wadau wengine wakifuatilia somo kwa umakini mkubwa sanaaaaaaa, wakuandika wako bize na wakusikiliza pia wako bize
Baada ya shule zote tatu kumalizika, Maza alikata keki ya Birthday yake ambayo ilikuwa inafuata siku ya jumatatu, the cake was really good na kila mtu alipata kipande. Happy birthday Mama NNN na wengine
Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment