I dont really remember ninini nilikuwa ninawaza hapa, but something funny was happening in her phone
Kuangaliana kwa smile mara nyingi kunazitoa nje hisia za ndani zilizojaa penzi baina yenu. Kuangaliana ana kwa ana kuna afya ya tofauti sana katika mahusiano yenu. Mara ngapi unapata muda wa aina hii na mpenzi wako?
Haichukui gharama kubwa kumfanya mwenzako a smile, ingawa ku smile kunategemea mambo mengi kama yamekaa sawa baina yenu. Tengenezeni mazingira ya hamasa kila wakati baina yenu, tabasamu la kweli litaibuka tu.
Iwe ni jukumu la kila mmoja wenu kuhakikisha mwenzake ana smile, katika kuonyesha hisia za ndani ndivyo utakavyozidi kumfahamu mwenzako kiuhalisia.
Wakati wowote tamani kuwa na muda naye, na upatapo muda huo na yeye uthamini, kuwa na kiu ya kuwa naye kokote, hii itakufanya kuzithamini hata dakika chache utakazopata kuwa naye sehemu. Kiu hii isiwe tu kwa mmoja bali kwenu wote, remember love is a two way traffic transaction.
Na mwishoni ndiyo tukagundua kuwa Emmanuel Mabisa alikuwa anafuatilia mazungumzo yetu na kupiga picha kwa siri bila sisi kufahamu. Thanks my good brother Mabisa for the wonderful photo moments.










0 comments:
Post a Comment