DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI. JINSI YA KUSHUHULIKIA MIGOGORO (HANDLING CONFLICTS). SEHEMU YA 1



Katika maisha yetu ya kilasiku, iwe kazini au ofisini au nyumbani, migogoro ni asili na sehemu ya maisha yetu. Ukweli ni kwamba maisha yangekosa uhalisi pasipo kuwa na migogoro hii. Hii husababishwa na ukweli kwamba hakuna anayefikiri, au kuwaza au kuwa na mtazamo sawa na mwenzake, kwa sababu vyanzo vya mitazamo hii hutofautiana kwa hali hii iko migogoro ambayo ni vigumu kuiepuka. Matatizo hutokea pale ambapo misunguano hii inaporuhusiwa kutoka nje ya uwezo wetu na kuzigusa haiba na hisia zetu. Vyanzo vya migogoro vyaweza kuwa vingi lakini kikumbwa ni kwamba kila mmoja anataka ushindi au kupenya kupitia njia yake, na hakuna aliye tayari kuafikiana na kuendana na mtazamo wa mwezake.
Baadhi ya sababu zinazo pelekea kuwepo na migogoro ni kama zifuatazo:-
-       Tofauti katika malengo
-       Ushindani – haswa unapozidi kipimo.
-       Kutokuwa na maelewano au tofauti za kimtazamo.
-       Kukosa ushirikiano – (Kihalisia au kwa kufikirika)
-       Migogoro ya haiba
-       Matatizo ya mamlaka – mfano misuguano na mabosi
-       Misongo binafsi ya mawazo
-       Uchu wa kutimiza majukumu
-       Kutokuwa tayari kukubali majukumu
-       Kushindwa kuishi au kufanya sawa sawa na mipango au maelekezo yaliyowekwa.
-       Tofauti katika namna au njia za kufikia malengo n.k.
Tafiti zimeonyesha kuwa wafanyakazi wengi (wasimamizi na wasimamiwa) hutumia zaidi ya asilimia 25 ya muda wao wakazi katika kusuluhisha migogoro. Jambo hili linaifanya migogoro kuwa ya gharama sana.
Migogoro sio jambo baya, mara nyingine ina matokeo mabaya na na nyingine ina matokeo mazuri, ile migogoro inayoleta matokeo mazuri lazima tujue jinsi ya kuichochea na kuiendeleza ingawa inabidi pia tuwe na ujuzi wa  kuvistahimili  vyema vile vyanzo vya migogoro hii ili visilete madhara yasiyotarajiwa.

Migogoro ya aina hii yaweza kuwa na faida zifuuatazo
-       kufunua vitu muhimu na vya msingi vilivyo fichika muda mrefu
-       kuboresha mawasiliano baina ya walengwa waliohusika.
-       Huchochea ari ya kazi na uwezo wa kufikiri.
-       Humwamsha kila mhusika kutimiza majukumu yake.
-       Huleta kufikiwa kwa suluhisho la tatizo au matatizo fulani
-       Huwawezesha wahusika kupunguza au kutua mzigo wa hisia au hasira zilizolundikana.
-       Huwawezesha wahusika kutumia ufanisi wao ili kuonyesha ujuzi walionao.
-       Kwa kawaida migogoro yenye matokeo mabaya haina budi kuepukwa ingawa sio rahisi mara zote. Hata kama kuna ugumu katika kuepuka migogoro basi jitihada za makusudi zifanywe ili kutafuta njia bora za usuluhishi.


Migogoro inaweza kuwa mibaya na inayoleta athari pale ambapo;
  1. Inaondoa akili na mawazo ya watu kutoka kwenye uhalisi wa jambo au mambo.
  2. Inasababisha mtu au kundi la watu kutoshirikiana.
  3. inapowafanya wanaohusika kuchanganyikiwa na kutoridhika.

Mtu yeyote anayeifahamu migogoro na kujua madhara yake anaweza kuwa na uwezo wa kuiepuka au kuisuluhisha. Wakati migogoro mingine ni ya kuiepuka, iko ambayo inabidi kuishuhulikia ili isije kuzidi na kwenda nje ya uwezo wetu. Ili kufanya hili liwezekane zingatia haya yafuatayo.
  1. Jifunze kutambua na kuzikubali tofauti baina ya watu. Mfano. haiba zao, mahitaji yao, historia zao, matumaini yao nk.
  2. Jifunze kusikiliza vema kila wengine wanachokisema na sio tu kukimbilia kutoa hukumu.
  3. Jaribu kuwafahamu vema wale wote ambao umekuwa unakwaruzana nao mara kwa mara, fanya hivi ukisha jielewa kwanza mwenyewe, na uelewe pia kwa nini wanafanya au wanakuwa vile walivyo.
  4. Jaribu kuangalia mambo kwa mtazamo wa wenzako pia, sio kila wakati kujiona uko sawa na wenzako ndio wanaokosea.
  5. Fahamu na ukubali kuwa haiwezekani kila mtu akubaliane na wewe mara zote, na usiruhusu hii hali ya kupingwa au kukosolewa kukukoseshe raha, na kukukasirisha.
  6. Waruhusu na wengine wanaohusika katika mgogoro wapate nafasi ya kujielezea vile wanavyofikiri, waombe wafanye hivyo kwa upole na sio kwa ukali.
  7. Baada ya mgogoro kutulia angalia nini umejifunza kutokana na mgogoro huo, usiruhusu mgogoro ukapita tu bila kujifunza chochote.
 Alhamis ya wiki ijayo katika sehemu ya 2 tutaangalia namna ya kuishuhulikia na kuipunguza migogoro hii, Usikose


Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment