MAN ENOUGH



Kutokana na mabadiliko makubwa ya kimaisha, kijamiii na kimtazamo kwa kiasi kikubwa sasa mwanaume huangaliwa kama MWANAUME kwa mambo mengi sana kama vile uwezo wake wa kuzalisha fedha, uwezo wake wa nguvu za mwili, uwezo wake wa kuwasilisha hoja, uwezo wake wa kuwa na wanawake wengi, uwezo wake wakukabiliana na matatizo na kuyashinda. Yako maeneo pia ambapo mwanaume huheshimika zaidi kulingana na gari analoendesha, nyumba aliyojenga, nyumba aliyowajengea wazazi wake, na mali alizonazo. Kwa hali yeyote ile uionavyo au uitafsirivyo wewe, bado mimi naona mitazamo yote hii haijakamilika na mingi ni potofu. Ninamuangalia mwanaume aliye MWANAUME kweli kama mtu mwenye uwezo wa kujaribu, mtu mwenye uwezo wa kuthubutu, mtu mwenye uwezo wa kuwa tayari kuitetea familia yake hususani kuwa tayari kumtetea mke wake, mtu mwenye uwezo wa kuilinda familia yake, hapa simaanishi ulinzi wa kuweka “fence” kwenye nyumba bali kuweza kuzilinda hisia za kila aishiye nyumbani kwake “emotiona protection”. Mtu mwenye uwezo wa kuongea mambo ya kujenga na ya kimaendeleo pamoja na familia yake na sio kwa siri wala kificho, mtu anayewasiliana vema na mke wake na watoto wake, mtu mwenye ujasiri wa kusimama na kuwaongelea vema watu wa familia yake wakati wowote na popote, na mwisho mtu asiyeona haya au aibu kuiweka mbele familia yake wakati wowote. This is a man enough – Chris Mauki
Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment