Hali hii inatokea ikiwa kama wewe mwanamke umemzidi mume wako, kielimu, kipato, kiakili, kifursa, kujulikana “fame”, au hata kama umetoka kwenye familia iliyo juu kidogo kifursa kuliko yeye. Yawezekana hatokwambia hata sikumoja lakini ndani ya moyo wake kuna mahangaiko makubwa sana mara anapowaza huo utofauti baina yako na yeye, yamkini pia wewe wala hauna wazo lolote baya na wala hautumii kipato, cheo, wala akili yako kumgandamiza lakini yeye wakati wote atawaza kuwa unafanya hivyo. Hii inaweza kuyasumbua sana mahusiano yenu, wako walioshindwa kushuhulikia jambo hili na wakajikuta wanatengana. Maneno ya mara kwa mara wanaume wa jinsi hii wanayoyasema ni kama vile; “Unajifanya na kamshahara kako hako ee??”, “Kamshahara kako kanakutia kiburi sio??”, “Au unafanya hivyo kwasababu mimi sina kipato kama chako??”, “Unakiburi kwasababu hii nyumba ni yako sio??”, “Unajifanya umesomaa??”, “Wewe hata kama una digrii yako hapa, mimi bado mume wako tu”, “Haijalishi wewe ni nani, na kwenu ni kina nani, hapa fahamu umeolewa tu, wewe ni mke tu hapa!!” Maneno haya na mengine ambayo yamkini umewahi kuyasikia au umewahi kuambiwa na mume wako, yakusaidie kufahamu kwamba hizo ni alama za “inferiority complex” - Chris Mauki
Kesho usikose, nitakuletea alama za kitabia anazozionyesha au kuzifanya mwanaume wa jinsi hii.

0 comments:
Post a Comment