JE UNALIJUA CHIMBUKO LA HIZO TABIA UNAZOZICHUKIA ZA MPENZI WAKO??


Pamoja na ukweli wa tafiti kwamba jinsi tunavyozielezea na kuzionyesha na kuzidhihirisha hisia zetu baina ya wanaume na wanawake au mke na mume hutegemea na utofauti tulionao katika maeneo ya ubongo wetu, ni kweli pia kwamba malezi na makuzi yetu yanachangia sana. Unapoona mtu anahasira za karibu, au haoni aibu kabisa, au analia kwa kitu kidogo, au ni mtu wakulaumu sana, au  mtu wa kutafuta  visingizio, au mtu wa kususa, au mtu wa kunyamaza na tabia nyingine nyingi, ujue malezi na makuzi yake yanamchango mkubwa sana katika kumfanya yeye kuwa hivyo alivyo. Usisahau au kutosisitiza kufahamu malezi na makuzi ya mwenzako kabla hamjaanza kuishi pamoja, yasije yakakutokea puani mengine usiyoyajua, ni bora hufahamu kuwa unaishi na chui kuanzia mwanzo kuliko kudhani unaishi na paka na baadae ukagundua kumbe ni chui – Chris Mauki


Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Mimi Nina hasira za karibu na ninapanic Mara kwa Mara ninapopatwa na tatzo mpaka nakera wa2 sometym..najaribu kuzuia but nashinda inatokea 2..please help me 2 know the source n how 2 control it..

    ReplyDelete