1. Je wewe ni katika wale wenye kujitoa, wakikwepa kuhusika katika mgogoro? (withdrawers)
Watu wanamna hii huwa na tabia ya kuiona migogoro kama si kitu, huiona migogoro ni ya kupoteza muda tu, haina haja ya kuchukua fikra zao nyingi, hawana haja ya kujiingiza katika kutatua. Hapa wanajitoa kimwili tu lakini kifikra na kihisia bado wapo ndani ya migogoro hiyo, kwa mfano; utaona mtu anaondoka katikati ya mazungumzo, kama mpo sebuleni mnaongelea kitu fulani ataondoka na kwenda kulala, kama mko chumbani anaweza kutoka kwenda kwa marafiki zake, au anajitoa kwa kutaka msiliongelee jambo hilo. Hujiweka katika hali ambayo itamfanya kila kinachoongelewa hakimwingii moyoni hata kama anakuangalia usoni, wengi wetu hutumia staili hii, ingawa sio tabia nzuri hata kidogo.
2. Je wewe ni katika wale wanaotafuta au kulazimisha ushindi katika mgogoro (winning)
Kama nafsi yako imetishwa na mgogoro huo, na unaona ni lazima ushinde wewe, basi kila wakati utalazimisha ushindi tu, kama wewe ni bosi au mwenye nafasi na mamlaka yako imeumizwa au kuguswa basi utakimbilia kulazimisha ushindi tu, haijalishi gharama au nani ataumizwa, kiu yako itakuwa kuibuka mshindi tu.
Watu hufanya mbinu mbalimbali ili tu kuwa washindi, kwasababu katika mahusiano tunajuana sana madhaifu yetu basi kila mmoja atajaribu kuingiza mkuki kwenye maeneo dhaifu ya mwenzake ili tu kumfanya mwenzake awe mpole na kuuruhusu ushindi uende kwa yule muumizaji. Ilikumshinda mtu muumizaji huyu atakutukana, atakukejeli, atakushushia hadhi, atakukumbusha historia yako ya nyuma yenye maumivu, atajaribu kuvigusa vidonda vyako vya zamani, anaweza akalenga pia madhaifu ya wazazi na ndugu zako na kuyahusianisha na mdhaifu yako, atajaribu tu kuvigusa vile vinavyoweza kukuliza ili tu ulie na yeye ashinde, nk.
3. Je wewe ni kati ya wale wenye kuamua kujishusha katika baadhi ya tofauti wakiagalia nani atafaidika na nini? (Compromizers)
Hapa mmoja huangalia eneo gani atafaidika kwa kujishusha na kukubali mawazo yake yashindwe, sio kila kitu atakuwa mpole, la! bali katika maneo fulani Fulani. Mtu wa hivi atakubali ajinyime kidogo ili basi afaidike kidogo na wewe ufaidike kidogo pia, sio kwamba ushinde kabisa, au ashinde yeye kabisa, staili hii huusisha wale wenye kuzifikiria pande zote mbili za mgogoro.
4. Je wewe ni kati ya wale wenye kutafuta suluhisho? (Resolvers)
Katika staili hii, wapendanao huruhusu mawasiliano ya wazi na ya moja kwa moja, katika kubadili hali, mtazamo au tabia zao, wapenzi wanakuwa tayari kutumia muda wowote kuziangalia tofauti zao, ili hata kama baadhi ya matakwa yao yametimizwa basi waridhike na suluhisho wanalolifikia pamoja.
Chris Mauki
chrismauki57@gmail.com

0 comments:
Post a Comment