PETE YA HARUSI KIDOLENI, KARAHA AU FURAHA??




Pete iliyoko kidoleni kwako sio ndoa, hiyo ni alama tu, haina mchango wowote kwenye uboreshwaji wa ndoa yako, ipo kama sticker ya urembo tu kwenye gari, ambayo ikiwepo au ikiondolewa haibadili chochote kwenye gari hilo. Ndoa ni matendo yako ya kila siku katika mahusiano yenu. Ni matendo ndiyo yanayoweza kuonyesha kama ndoa yenu ipo au haipo hata kama watu wanaowazunguka wanaiona kama vile ipo. Pete kidoleni haiwezi kukupa amani na furaha moyoni, bali matendo yako au ya mwenzako ndiyo yanayoweza kukupa amani na furaha au badala yake kukupa karaha. Pasipo kuboresha jinsi unavyoishi kwenye hiyo ndoa yako hakutatokea mabadiliko yeyote kamwe, na furaha ya ndoa utaisikia kwa wengine tu. Hii haijalishi hata kama pete yako ina dhahabu ya uzito wa kilo nzima. Ukifanikiwa kuwa na furaha na amani na mumeo au mkeo, pete inabaki kama alama ya kile chema mnachokiishi. “Remember that your wedding ring changes nothing, your actions into the marriage does” - Dr. Chris Mauki
Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment