Ni ngumu sana kujaribu kumbadilisha mtu alivyo pasipo kwanza kubomoa au kuharibu jinsi alivyokuwa hapo awali. Kabla ya kukurupuka na mikakati ya kumbadilisha huyo mpenzi wako na hizo tabia zake unazoziona mbaya, je umeshawahi kujiuliza zilianzia wapi? Je niwangapi wameshapata shida na tabia zake hizo? Je waliowahi kujaribu kumsaidia kubadilika walishindwa wapi? Je yeye anayakubali na yuko tayari kuyapokea mabadiliko? Au wewe ndiyo unataka kulazimisha mabadiliko hayo. Kumbuka wakati wote kuwa kiumbe binadamu ni mwenye tabia ngumu na zinazobadilikabadilika kufuatana na muktadha “context”, ili kuleta au kuandaa mabadiliko ya kweli na yatakayodumu mwenye tatizo la kitabia hana budi kulifahamu tatizo lake na kukubali kuwa tayari kushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya tabia. Kama unahangaika kumbadilisha tabia mtu ambaye wala hajui kama tabia aliyonayo ni tatizo basi ni bora na yule aliyeamua kuufukuza upepo. “Human behaviour is a complex thing” - Chris Mauki
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment