UKITAKA KUIJUA HALI YA NDOA USIMUULIZE MWANAUME



Ni mara nyingi sana na kuna uwezekano mkubwa sana kwa mwanaume kuona, kufikiri, au kudhania kuwa ndoa au mahusiano yake yako sawa kabisa na hayana tatizo lolote, tena anaweza kujigamba na kujisifu kabisa kwa hilo, wakati kwa upande mwingine mke wake anajisikia uchungu moyoni mwake na kukiri kwamba ndoa yao inawaka moto na yamkini mwanamke huyu anatamani hata watengane. Yako mambo madogo madogo sana kwenye mahusiano wanaume huyafumbia macho au kutokuyaona umuhimu wake kabisa huku wakidhani hali ni shwari, kinyume chake wake zao wakiyaangalia mambo hayo wanatamani ndoa ipasuke ili wapate pumziko. Labda umewahikuona ndoa nyingine kila kitu kinaonekana kiko sawa, mke na mume kwa nje mambo shwari wanaishi pamoja kwa miaka mingi tu na ghafla unasikia wametengana, halafu unashangaa nini kimetokea. Hapa inamaana mwanandoa mmoja kabanwa pumzi muda mrefu sana bila mwenzake kufahamu uhalisi wa maumivu ya mwingine. Hii imenifanya kujifunza kuwa, mtu sahihi wa kumuuliza hali ya ndoa au mahusiano (kama yanafuraha au kama yanamachungu) sio mwanaume bali ni mwanamke – Chris Mauki.
Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment