PRESSING THE RIGHT BUTTON Baraka Kiranga 12:09 AM Mahusiano Edit Neno kujali “to care” (‘anajali’ ‘hanijali’) linatofauti sana kwenye mtazamo wa mwanaume na mwanamke. Nakupa mfano, wewe mwanaume ukituma fedha kwa wazazi wa mkeo ili mkeo afurahi unavyowajali wazazi wake wewe unahesabu tendo hili ni kumjali na kumpenda mkeo wakati yeye kwa mtazamo wake wala haoni umemjali yeye bali umewajali wazazi wake. Unapoamua kuwa makini kujaza friji yenu vyakula na kuhakikisha watoto na familia wako sawa kila wakati, wewe unahesabu umemjali mkeo, yeye anaona unawajali watoto wako. Tofauti na kufanya hivyo, unapomwambia “umekula mpenzi?”, “hiyo nguo imekupendeza sana” “samahani kwa neno nililosema” (hatakama haumaanishi) kwake huko ndiko kujali. Wewe mwanaume, chunga sana ili juhudi zako zote za kuonyesha unajali zisije kuishia kwenye “dust bin” halafu ukaumia moyo pale utakapoambiwa kuwa hakuna unachokifanya hata kimoja. “Learn to press the right button, not just any button” – Chris Mauki. Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Baraka Kiranga This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Post a Comment