Wakati mwanamke anahesabu kupendwa na kuonyeshwa penzi ni pale mwanaume anapoonyesha kuwa anamuelewa, anamjali, anajali hisia zake, kama vile kufahamu nyakati ambazo mkewe ameumia moyo au anapofurahi au anapokuwa katika tatizo fulani. Tofauti na mwanamke, mwanaume hudhani kuonyesha upendo kwa mkewe ni kutoa ufumbuzi wa haraka pale mkewe anapomkimbilia kutafuta ufumbuzi wa tatizo, kwa kufanya hivi mke wake anaongeza kulia na kulalamika kwamba mume wake hajali hisia zake, na kwa kuongeza kulia na kulalamika mume anamlaumu mke wake kuwa ni mtu wa ajabu, asiyetaka kusaidika na anaye fanya mambo kama mtoto mdogo “Crazy cycle”. Labda niwasaidie wanaume hapa, wewe mwanaume kabla hujakurupuka kutafuta suluhisho la tatizo lolote, ruhusu kwanza kinywa chako kionyeshe kuwa unakubali na kufahamu “you acknowledge” maumivu ya mke wako au hisia zake kwa ujumla, hiyo yaweza kuwa dawa tosha kwake kuliko huo utatuzi utakaokuja nao. “Sometimes care costs nothing” – Chris Mauki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment