Wote tulisubiriana Boko magengeni sheli ya Oil om kabla ya kuanza kuelekea Oceanic, huyu ni Protas Godwin na mkewake
Mara tu baada ya kufika Oceanic Mbweni
(Kulia kwangu) Chris na Miriam, Dr Tandi wa Adelard, Adeline wa Allen, na Maggy wa Henry. (Nyuma) Adelard, Protas, Henry, na mwisho ni mke wa Protas
Tumefika na tumeketi tukisubiri vinywaji na msosi
Maakuli na madrinks yakiendelea, hapa ni mwendo wa kuku choma, bata choma, kanga choma, na mbuzi
Baada ya maakuli tukabadilisha mkao, tukaenda kwenye discussion table, hapa tunadadavua na kujadili kwa kina changamoto zilizopo katika ushiriki wa kila mwanandoa kwenye uchumi wa familia, hapa kidogo pachimbike jana, watu hawakuogopa manyunyu, usiku kuingia, wala kuchelewa nyumbani hadi kieleweke
Protas hapa anatoa macho na kusikiliza kwa makini, mkewe akichangia mada jinsi mume alivyo na wajibu wa kumshirikisha mkewe mapato na vyanzo vya mapato hayo, hapa unakuwa mpole manake unaweza kushushuliwa na maiwaifu wako hadi ukimbie, ni uwazi bin openness, na wote tunajengana
Kama kawa nipo makini kusimamia mjadala uende poa na watu wasije toana macho, manake sometimes pananoga kweli
Very attentive
Kaka Nkya, mzee wa THT na Miriam wa mimi wakifuatilia discussion









0 comments:
Post a Comment