Maranyingi unapoongea na mpenzi wako wa kiume au mume wako na ukaona kama hakuelewi ingawa anakuangalia, unamshangaa na labda kumkasirikia, yamkini hujui kwamba tatizo walilonalo wanaume mara tu unapoanza kuongea naye kabla hujamaliza kuongea unachokiongea tayari unakuta sehemu ya ubongo wa wake inayoshughulika na kutafuta suluhisho la matatizo “analyze and fix it circuits” huamka gafla na kumfanya awaze namna gani ya kutatua tatizo lako (yaani hapa ubongo wa mwanaume hutafsiri kwamba kila kinacholetwa mbele yake ni tatizo na hivyo linahitaji kutatuliwa), kwa kule kutojua kwako wewe mwanamke labda utanyamaza kuongea au kumkasirikia, au atakuudhi kwa vile atakavyorukia kutaka kukupa majibu hata kabla hujamaliza kuongea na hapo magomvi na tofauti nyingi huibuka na badala yake wanawake huenda kueleza kitu kile kile kwa mama au dada zao au rafiki yeyote wakike, na kwasababu wao ni jinsia moja, yani anakwenda kuongea na wanawake wenzake, na kwasababu mfumo wa ubongo wao unafanana huyu mwenye kuelezea jambo atajiona amesikilizwa na ameeleweka, na atafurahi, (hii ni kwasababu wanawake wanaweza kusikiliza kuliko wanaume), mara mwanaume atakapogundua kuwa mke wake amezungumza mambo ya ndani kwa ndugu zake wa kike au kwa rafiki zake vita inaibuka tena na hapa ndipo kupigwa marufuku kuongea na ndugu zako au rafiki zako kunapoanza. Ukiangalia mzunguko huu mzima hakuna aliyejua kwanini anafanya vile anavyofanya, madhara yake ni nini, na ni kwajinsi gani anaweza kumsaidia mwenzake. Mwanzoni mwanamke alimkasirikia mwanaume akimtuhumu kwamba hamsikilizi bali anakurupuka tu kuongea na kutoa hitimisho “conclusions”, na baadae mwanaume akamkasirikia mwanamke akimtuhumu kwamba anaongea na watu wa nje mambo ya ndani badala ya kuongea na yeye kwanza. Hii “crazy cycle” inaweza kuwafanya mkaachana kama msipokuwa macho. Nivema tukijua tofauti tulizonazo na jinsi zinavyoweza kuathiri mahusiano yetu – Chris Mauki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment