Siku moja kabla ya valentine day tar 13.2.2015 tulipata nafasi ya kushiriki katika Pre-valentine lovers dinner and talk pale New Arusha hotel. Kwakweli ilikuwa poa sana, chakula, mandhari, talk na mahudhurio vyote vilibamba sanaaaa. Shukrani za pekee zimuendee dada nangu Salmka Mnaro wa Ali aliyekuwa injini kubwa katika kubeba maono na kuiandaa shuhuli hii Arusha pamoja na vipingamizi na changamoto tele alizokutana nazo. Picha hizi chache zitakupa picha ya ishu nzima. Endelea
Hapa muandaaji Salma akifanya ufunguzi na kuelezea nia nzima ya tukio hili
Salma Mnaro wa Ali akidadavua kidogo kuiweka bayana event hii kwa waalikwa
Wapendanao wakisikiliza kwa makini
Dr. Chris Mauki na Mke wake Miriam wakiwa wenye furaha sana kabla ya kusimama kuzungumza
Salma katika buffe
Salma na mume wake Ali mwenye shati jeupe wakifuatilia kwa makini talk kutoka kwa Dr. Chris
Salma akishukuru kwa yote, pembeni yake ni Miriam wa Mauki na MC wa shuhuli
Shuhuli ilienda sawia haswa kwenye maakuli
PICHA ZIFUATAZO NI MATUKIO KABLA NA BAADA YA TUKIO
Hivi ndivyo ukaribisho ulivyokuwa baada tu ya kukanyaga sakafu za chumba ndani ya Mount Meru Hotel Arusha
Asubuhi tukiwa tuna check out hotelini kukimbilia uwanja wa ndege wa KIA kuanza safari ya kurudi Dar ambako maandalizi ya Valentine Lovers Dinner n Talk yalikuwa yakiendelea
Miriam wa mie akiwa amepozi hotelini
Kweli milima haikutani, tukiwa kwenye lunch Mount Meru Hotel tukakutana na rafiki yetu wa muda mrefu Salome Pangamawe, tena yeye akiwa ni kiongozi katika hoteli hiyo.
Hapa nikikamilisha taratibu za ku cheki in hotelini
Hii ni view tokea room kwetu hotelini Mount Meru





0 comments:
Post a Comment