Elewa kwamba mahusiano yako au ndoa yako ni kazi au jukumu linayoendelea, siyo kazi au jukumu lililomalizika au litarajiwalo “your relationship is a work in progress”. Hii haijalishi vipindi vya magumu au tambarare mnavyovipitia kama wanandoa au kwenye mahusiano hayo. Kila siku iitwayo leo, kila mmoja wenu hana budi kutia jitihada na juhudi katika kuhakikisha anaboresha hali ya mahusiano yenu, jukumu hili ni la kila mmoja na haitakiwi mmoja kudhani kwamba ni jukumu la mwingine na yeye hahusiki kabisa. Wote nyie ni wadau wenye hisa sawa katika mahusiano yenu. Usikae kwenye mahusiano na mwenzako kama vile yeye ndiyo anafaidika zaidi kwa kuwa na wewe, na kwa hivyo yeye ndiyo ajitahidi kuhakikisha mnaishi vema pamoja, usifikiri kwamba kwa kuishi naye, yeye ndiyo anafaidika zaidi, huo sio mtazamo mzuri. Fahamu tu kwamba mahusiano haya yanawahusu wote wawili, faida na hasara zake ni zenu wote – Chris Mauki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment