KWA WALE WANAODHANI WANACHUMBIWA: JIULIZE KWANZA Baraka Kiranga 9:48 PM Mahusiano Edit Ewe dada unapokuwa kwenye mahusiano na mwanaume kabla ya ndoa, hatakama amekuahidi kukuoa au ameshakutambulisha kwao au hata kukuvisha pete, au kukuahidi vingine vingi usisahau kwamba wanaume mara nyingi wanafanya usahili “interview” kabla ya kuoa, na hapo wao humpata mmoja wa kumuoa, na mara nyingine hata hawana uhakika wa kama huyo waliyemchagua kumuoa atamfaa au hatomfaa. Unaweza kudhania kuwa wewe ndio mke mtarajiwa mteule kumbe kwake yeye wewe ni mmoja wa watahiniwa, na hauko peke yako, ndio maana wengi huumizwa nyakati za mwisho wakidhani wangeolewa na kujikuta anaolewa mwingine. Hembu jaribu kumuuliza huyo mpenzi wako wa kiume, ambaye labda amekwambia kuwa anakuchumbia, muulize “je upo hapa kwa ajili ya kumuandaa mke wako au mimi ni mmojawapo ya wanaofanyiwa “interview”?? – Chris Mauki Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Baraka Kiranga This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Post a Comment