DOZI YA JUMAMOSI: KAMA HUJUI JIFUNZE Baraka Kiranga 10:30 PM Mahusiano Edit Kumlinda na kusimama upande wa mke wako dhidi ya mawimbi ya ndugu au rafiki zako ni jukumu la mwanaume yeyote. Mwanaume asiyefanya hivyo au anayefanya tofauti na hivyo ama hajui jukumu lake, hajui uthamani wa mke aliye naye au hafahamu hata kidogo madhara ya tabia yake ya kutomlinda mkewe na kusimama upande wake “come what may”. Sikatai kwamba mara nyingine yako mambo utatofautiana na mpenzi wako, ila tofauti zentu katika jambo hilo zishuhulikiwe mkiwa peke yenu na sio mnapokuwa na watu, ndugu au marafiki na ukijionyesha wazi kwamba hauko upande wake bali upande wa maadui zake. Hii huwa mbaya zaidi pale unapokuta umeegemea upande wa ndugu zako na kumwacha mkewako “unayedai kuwa ni mpenzi wako” akiwa amesimama pekeyake. Hata kama ni mama yako au baba yako, jifunze kuruhusu nguvu ya penzi kumfunika mkeo, na wanaojaribu kumvamia hisia zake wajue analindwa. Kwani ulidhani kuwa mume ni kufuliwa, kupikiwa na kuzalisha tu?? Na kama mengine ya muhimu ulikuwa hujafunzwa, mbona ulikimbilia kwenye maji usiyoyaweza?? “Take your responsibility Mr Man, being a Man is more than wearing a pair of trouzers” – Chris Mauki Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus About Baraka Kiranga This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel. RELATED POSTS
0 comments:
Post a Comment