KWA WANAUME


Hii ndio kauli inayorudiwa mara nyingi sana ninapoongea na karibu kila mwanamke ambaye suala lake lina husiana na mahusiano yake na mpenzi wake. “Natamani ……………… (weka jina lako hapo wewe mwanaume) anisikilize, natamani anikumbatie, natamani anieleze jinsi anavyozijua hisia zangu na jinsi mimi anavyojisikia kuhusu mimi, natamani awe wazi kwangu kuhusu nafasi yangu moyoni mwake, badala yake kila siku yeye anakuwa kama roboti tu, ananyamaza tu, na kama akizungumza basi ni kunielekeza nini chakufanya na nini sicho chakufanya, yani kama vile alivyokuwa anafanya baba yangu au mwalimu wangu”. Mimi naamini mabadiliko ni kitu kinachowezekana, kama kweli unampenda mkeo au huyo mpenzi wako na unamhitaji basi furahisha hisia zake au kama umemchoka na haumhitaji basi kuwa muwazi umwambie ajue kwamba yeye ni “reject”au ni “unwanted material” kuliko kumweka kituo cha basi akisubiri basi ambalo halipo na kamwe halitakujaChris Mauki
Share on Google Plus

About Baraka Kiranga

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment